Thursday, August 18, 2016

CHAPATI ZA SAMLI

                                                         

CHAPATI ZA SAMLI

MAHITAJI
Ngano kilo 1, mafuta ya kupikia vijko 4 vya chakula, sukari vijiko 2, chumvi kijiko 1, 1% butter milk 400 mls (unaweza kutumia plain/natural yoghurt 200 mls, maji ya uvuguvugu na small (ghee) au margarine/ butter yoyote.

JINSI YA KUANDAA
Weka unga kwenye chombo cha kukandia, weka chumvi na sukari changanya vizuri, pasha mafuta ya kupikia yawe ya moto kabisa, yamwagie kwenye unga wako changanya na mwiko ili usiungue vidole, yakipoa kidogo pekecha mabonge ya unga mpaka yaishe unga uwe mlaini. 
Mimina butter milk au plain yoghurt au mtindi kisha changanya vizuri. Anza kuongeza maji ya uvuguvugu kidogokidogo huku ukikanda unga mpaka uwe laini (hapa ndo kuna siri usiwe mvivu, kanda dakika 10, acha kama dakika 5, kanda tena dakika 5), kata madoge madogo 12-13. 
Chukua donge mojamoja anza kusukuma, paka samli robo kijiko kisha kunja. Ukimaliza hatua hiyo funika hayo madonge uliyokunja na kitaulo safi kwa nusu saa (unafunika ili yasikauke). Anza kuchoma chapati zako, kama kikaango sio cha kushikia (non-stick) weka chapati uliyosukuma bila mafuta kwanza, ikianza kubadilika rangi geuza upande wa pili kisha ndo uweke mafuta kidogo tu (upishi sio mafuta!!!) chapati inayoiva vizuri hadi ndani utaona inafura juu kama puto. Enjoy!!!

4 comments: