ANDAZI LA NGANO ISIYOKOBOLEWA
MAHITAJI
*Ngano 500g
*Mayai 2 (yapige mpaka povu)
*Baking powder (CHAPA MANDASHI nzuri zaidi) kijiko cha chakula 1
*Hamira kijiko cha chakula 1
*Mafuta ya kula vijiko vya chakula 2
*Iliki (ukipenda) kijiko cha chakula 1 (weka zile punje nyeusi kwenye sufuria kavu jikoni geuzageuza kama dakika 1 kisha twangwa zikiwa fresh, sipendi ile ya unga).
*Sukari kiasi upendacho
*Maziwa fresh ya baridi ya kukandia
JINSI YA KUANDAA
WEKA UNGA NA VITU VYOTE VIKAVU KWENYE BAKULI CHANGANYA VIZURI. WEKA MAYAI KANDA. WEKA MAFUTA YA KULA KANDA. ANZA KUWEKA MAZIWA TARATIBU HUKU UNAKANDA MPAKA UPATE LILE DONGE UNALOHITAJI. ANGALIZO: UNGA WA MAANDAZI UWE MGUMU KIASI KULIKO WA CHAPATI AU SKONZI MAANA UKIUMUKA UNALEGEA ZAIDI HIVYO MAANDAZI YATANYONYA MAFUTA UKICHOMA. UKIMALIZA KUKANDA (BAADA YA DAKIKA KAMA 10, FUNIKA DONGE LAKO NA KITAULO KISAFI ACHA KAMA NUSU SAA, KANDA TENA KWA DAKIKA 5 KISHA FUNIKA TENA ACHA UUMUKE UWE MARA 2. KATA UMBO UPENDALO, CHOMA.
Bi Moremi, asante sana kwa maelekezo yako. Ingawa nina swali, hivi kuna tofauti nisipotumia maziwa?
ReplyDeleteBi Moremi, asante sana kwa maelekezo yako. Ingawa nina swali, hivi kuna tofauti nisipotumia maziwa?
ReplyDeleteWewe ni noma aisee nimekushindwa
ReplyDeleteBig up sana
Ngano nkinunua nakusaga mwenyew itafaa maana sehem nyingine kupata unga huu ni shida na cjawah kuuona dukan
ReplyDeleteNgano nkinunua nakusaga mwenyew itafaa maana sehem nyingine kupata unga huu ni shida na cjawah kuuona dukan
ReplyDelete