Thursday, August 18, 2016

MARINATION YA NYAMA YA KUCHOMA


MAHITAJI
Nyama 1 kg, Buttermilk 250 mls (waweza kutumia mtindi), limao 1, tangawizi (grated) vijiko 2, them vijiko 2, pilipilimanga kijiko cha chai 1, curry powder kijiko 1, garam masala kijiko 1 na turmeric powder kijiko 1 (ukiweza kupata fresh ni bora zaidi ikwangue (grate) kama tangawizi, mafuta ya kupikia kijiko 1 (natumia Olive oil), chumvi kiasi upendacho.

JINSI YA KUANDAA
Changanya vitu vote kwenye bakuli isipokuwa chumvi na limao  Mchanganyiko ukiwa tayari weka nyama changanyanya vizuri kisha kamulia limao, weka chumvi changanya tena. Weka nyama kwenye mfuko wa plastic funga vizuri weka kwenye friji masaa 2 mpaka 6 (inategemea unataka kuchoma saa ngapi). Ukiwa tayari choma, tengeneza kachumbari ya kiswahili (nyanya, kitunguu, ndimu, na chumvi), Enjoy!!!

CHAPATI ZA SAMLI

                                                         

CHAPATI ZA SAMLI

MAHITAJI
Ngano kilo 1, mafuta ya kupikia vijko 4 vya chakula, sukari vijiko 2, chumvi kijiko 1, 1% butter milk 400 mls (unaweza kutumia plain/natural yoghurt 200 mls, maji ya uvuguvugu na small (ghee) au margarine/ butter yoyote.

JINSI YA KUANDAA
Weka unga kwenye chombo cha kukandia, weka chumvi na sukari changanya vizuri, pasha mafuta ya kupikia yawe ya moto kabisa, yamwagie kwenye unga wako changanya na mwiko ili usiungue vidole, yakipoa kidogo pekecha mabonge ya unga mpaka yaishe unga uwe mlaini. 
Mimina butter milk au plain yoghurt au mtindi kisha changanya vizuri. Anza kuongeza maji ya uvuguvugu kidogokidogo huku ukikanda unga mpaka uwe laini (hapa ndo kuna siri usiwe mvivu, kanda dakika 10, acha kama dakika 5, kanda tena dakika 5), kata madoge madogo 12-13. 
Chukua donge mojamoja anza kusukuma, paka samli robo kijiko kisha kunja. Ukimaliza hatua hiyo funika hayo madonge uliyokunja na kitaulo safi kwa nusu saa (unafunika ili yasikauke). Anza kuchoma chapati zako, kama kikaango sio cha kushikia (non-stick) weka chapati uliyosukuma bila mafuta kwanza, ikianza kubadilika rangi geuza upande wa pili kisha ndo uweke mafuta kidogo tu (upishi sio mafuta!!!) chapati inayoiva vizuri hadi ndani utaona inafura juu kama puto. Enjoy!!!

Thursday, August 4, 2016

ANDAZI LA NGANO ISIYOKOBOLEWA



ANDAZI LA NGANO ISIYOKOBOLEWA

MAHITAJI 

*Ngano 500g *Mayai 2 (yapige mpaka povu) *Baking powder (CHAPA MANDASHI nzuri zaidi) kijiko cha chakula 1 *Hamira kijiko cha chakula 1 *Mafuta ya kula vijiko vya chakula 2 *Iliki (ukipenda) kijiko cha chakula 1 (weka zile punje nyeusi kwenye sufuria kavu jikoni geuzageuza kama dakika 1 kisha twangwa zikiwa fresh, sipendi ile ya unga). *Sukari kiasi upendacho *Maziwa fresh ya baridi ya kukandia


JINSI YA KUANDAA 

WEKA UNGA NA VITU VYOTE VIKAVU KWENYE BAKULI CHANGANYA VIZURI. WEKA MAYAI KANDA. WEKA MAFUTA YA KULA KANDA. ANZA KUWEKA MAZIWA TARATIBU HUKU UNAKANDA MPAKA UPATE LILE DONGE UNALOHITAJI. ANGALIZO: UNGA WA MAANDAZI UWE MGUMU KIASI KULIKO WA CHAPATI AU SKONZI MAANA UKIUMUKA UNALEGEA ZAIDI HIVYO MAANDAZI YATANYONYA MAFUTA UKICHOMA. UKIMALIZA KUKANDA (BAADA YA DAKIKA KAMA 10, FUNIKA DONGE LAKO NA KITAULO KISAFI ACHA KAMA NUSU SAA, KANDA TENA KWA DAKIKA 5 KISHA FUNIKA TENA ACHA UUMUKE UWE MARA 2. KATA UMBO UPENDALO, CHOMA.