Saturday, January 7, 2017

PANCAKES ZA UNGA WA MCHELE

MAHITAJI
2 mugs unga wa mchele
2 mugs tui bubu (tui la nazi la kwanza)
2 tablespoons ngano
1 teaspoon iliki  (iliyosagwa)
1 tablespoon (flat) amira
1 yai
1/2 mug sukari.

JINSI YA KUANDAA
Changanya unga wa mchele na tui la nazi kwenye bakuli upate uji mzito. Ongeza amira, iliki na unga wa ngano changanya tena kisha uache uumuke (utaona umefura na vitobo tobo vya hewa).
Ukiumuka changanya lile yai na sukari pembeni kisha changanya kwenye unga acha kidogo uumuke kisha choma.
Ukiwa na kikaango kisichoshika (non-stick pan) huhitaji mafuta hata kidogo. Nimechoma zangu bila mafuta.

TIP: Recipe hii pia unapata vitumbua bomba.

No comments:

Post a Comment