Sunday, December 4, 2016

GUACAMOLE

MAHITAJI
Parachichi (Avocado) zilizoiva vizuri 2
Thomu (Garlic cloves) 2 (iliyotwangwa/ minced/ grated)
Kitunguu maji cha wastani nusu (kata cubes ndogondogo sana)
Nyanya 1 (Kata cubes ndogondogo)
Ndimu busu
Giligiliani (coriander leaves) zilizokatwakatwa vijiko vya chakula 2
Mfinyo wa chumvi (pinch of salt) na pilipilimanga (ukipenda)

JINSI YA KUANDAA
Menya parachichi kata vipande vidogovidogo weka kwenye bakuli safi. Chukua mwiko au potato masher anza kupondaponda (unaweza kutumia blender ya mkono ila litalainika sanaaa) raha yake liwe na ugumu kiasi.
weka thomu, kitunguu maji na giligiliani changanya vizuri na mwiko. Ongeza nyanya kisha kamulia ndimu, kama hupendi ndimu nyingi kamulia kiduchu ila usiache kabisa hii ni muhimu sana kwa ladha ya ukweli.
changanya vizuri kama unasonga ugali, ongeza ka chumvi na pilipilimanga ukipenda, changanya tena. Enjoy kwa kupaka juu ya mkate, chapati au kula na viazi vitamu kama mimi nipendayo.