Sunday, November 13, 2016

SUPU YA KONGORO (COW LEGS SOUP)



MAHITAJI
Makongoro (cow legs)1kg, leeks 1, Irish potato (viazi ulaya) 2, karoti 1, pilipili boga (hoho) 1, chumvi na pilipilimanga kiasi upendacho.

JINSI YA KUANDAA
Osha makongoro weka kwenye sufuria safi, ongeza maji yawe mara 2 level ya makongoro. Teleka sufuria jikoni, yapike mpaka yaive (dakika 30-45). Unaweza kulazimika kuongeza maji mpaka uhakikishe yameiva vizuri.
Sambamba; Kata leeks hiyo sehemu nyeupe vipande vidogo sana, osha vizuri weka kwenye sufuria safi. Kata viazi mkato wa cubes ndogondogo changanya na leeks kwenye sufuria weka chumvi kiasi na maji glass 3. Teleka sufuria jikoni vichemke kwa dakika 15, kisha ongeza karoti na hoho ulizokata cubes ndogondogo vichemke kwa dakika 8-10, epua tumia blender (nimetumia ya mkono) kusaga ziwe kama ndizi za mtori. Changanya kwenye makongoro yaliyoiva ongeza pilipilimanga, acha vichemke pamoja kwa dakika 5 na supu itakuwa tayari. Enjoy